Ufundi Useremala

Jifunze kutengeneza samani, milango, madirisha, na miundo ya mbao kwa kutumia vifaa na teknika za kisasa. Kozi inayokupa ujuzi wa kutosha kujiajiri au kuajiriwa.

Jiunge Sasa

Kwa Nini Chagua Kozi ya Useremala?

Kozi yenye mkazo kwenye mafunzo ya vitendo na ujuzi wa kutengeneza miundo thabiti ya mbao.

Karakana ya useremala

Karakana ya Kisasa

Chuo kina karakana iliyo na vifaa vya kisasa kama mashine za kukatia, kuchonga, na kupima mbao ili ujifunze kwa vitendo na ufanisi.

Wakufunzi wa useremala

Wakufunzi Wenye Uzoefu

Wakufunzi wetu ni mafundi wakongwe wenye uwezo wa kukuongoza katika kutengeneza samani zenye ubora na uimara.

Mafunzo ya Ujasiriamali

Utafundishwa jinsi ya kuanzisha na kuendesha karakana au biashara ya useremala, upangaji wa bei, na usimamizi wa wateja.

Uunganishwaji na Makampuni

Tunakuunganisha na karakana za useremala na viwanda vinavyotengeneza bidhaa za mbao kwa mafunzo ya vitendo na uzoefu wa kazi.

Mtaala / Moduli za Kozi

Kozi imegawanywa katika moduli rahisi zinazokupa ujuzi wa hatua kwa hatua.

Moduli 1: Msingi wa Useremala

Utambulisho wa vifaa vya useremala, aina za mbao, usalama wa kazi na matumizi sahihi ya zana.

Moduli 2: Ujenzi wa Miundo Midogo

Kutengeneza kazi ndogo kama meza ndogo, fremu na miundo rahisi kwa kutumia vipimo sahihi.

Moduli 3: Samani na Ubunifu

Kutengeneza kabati, vitanda, meza, makabati ya mambo ya ndani na bidhaa zingine za mbao.

Moduli 4: Mashine na Teknolojia za Kisasa

Kutumia mashine kama circular saw, planner, router, belt sander na nyinginezo.

Moduli 5: Ujasiriamali kwa Mafundi Useremala

Utajifunza bei, kuandaa ofa, kutafuta wateja, usimamizi wa vifaa, na ubunifu wa bidhaa.

Mafunzo ya Vitendo na Uzoefu wa Kazi

Mazoezi ya karakana na attachment vitakuandaa kuingia sokoni kwa kujiamini.

Jiunge na Kozi Leo

Udahili unaendelea — pata maelezo ya ada, mtaala na tarehe za kuanza kwa kuwasiliana nasi.

Jiunge Leo Rudi Mwanzo

Mawasiliano

Kwa maelezo ya kozi au utaratibu wa kujiunga, wasiliana nasi.

Ofisi ya Udahili - IVTC

📍 Mafinga-Iringa, Mkabala na Benki ya MUCOBA

📱 0754 271181 | 0717 435333

📧 incometvtc@gmail.com

Maswali ya Kozi

Kwa ada, mtaala wa kina na ratiba ya masomo, tuandikie barua pepe au tembelea ofisi.

Muda wa kazi: Jumatatu – Ijumaa, 8:00AM – 4:00PM